Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

BELIEVE THE GOSPEL (IAMINI INJILI)

NAOMBA TWENDE PAMOJA KUHUBIRI INJILI. NA EV PETER KAMANIJA.

 
Baada ya Mungu kunipa maono ya kuhubili na kufundisha Duniani kote ikiwa ndio ujumbe mkuu kuwaambia watu ukweli wa injili nikawa sina jinsi zaidi ya kuanza  mipango na mikakati ya kuhakikisha alichonipa Bwana katika maono yake kinatimizwa kwa namna yoyote ile na kwa ghalama yoyote ili kufanikisha ujumbe huu wa Injili kuenea kwa hakikisho na utibitisho mkubwa wa Roho Mtakatifu. Kama Biblia isemavyo. utawezaje kutulia ikiwa BWANA amekupa agizo?” Yeremia 47:7.
Ndugu yangu  mpendwa katika Bwana tafadhali sana usomapo ufahamu kwamba Dunia yetu hii inamhitaji Mungu sana. Watu wanahamu kubwa ya kulisikia NENO LA MUNGU kuliko vile tunavyofikili. Hebu pata hamasa kubwa ya kuhakikisha ujumbe huu wa Kristo unahusika kwa kiasi kikubwa kuupeleka, tunawasema wazungu wanabarikiwa ni kwa sababu wako bize na kujitoa kwa ajili ya kazi ya Mungu kwa namna yoyote wanayoweza. Mpendwa je si zaidi na kwangu Mimi na wewe tukijitoa kabisa kwa Mungu? Hakika Mungu hatakuacha atakubariki kwasababu umeugusa moyo wa Mungu.
Ndugu yangu mpendwa huduma hii ya Injili inahitaji  vitu vingi mno hakuna kitu utakacho kitoa kisiwe na kazi hata shilingi miamoja ina thamani kubwa mno. Tena usizalau.
Nimesema hivyo kwani huduma hii hasa niya vijijini, hebu angalia ndugu yangu  ni asilimia ngapi ya wahudumu wanao hubiri injili vijijini? Au wale wa vijijini wanatiwa moyo na akina nani? Tafadhali nyanyuka na mimi twende vijijini kuipeleka injili.
Siku moja mke wangu alimsikia mtu mmoja akisema katika kijiji furani toka nimefika hapa sijawahi kuona mkutano wa Injili”  kufuatilia kijiji hicho kwa mda wa huyo mtu ni miaka zaidi ya mitatu. Kwa mda huo Mijini imehubiliwa mikutano Mingapi? Moyo wangu unaniuma sana kiasi kwamba naona wakiniita “njoo na huku vijijini tunahitaji kuisikia injili”.
Moyo wangu unaripuka kwa moto mkuu, wa kuona vijiji vinakombolewa kwa Damu ya Yesu Kristo.
Mpendwa niwezeshe niipeleke Injili kisha taarifa nitakuwa naiweka wazi katika blog hii ili na wewe uone mambo ambayo mungu anafanya kupitia mkono wako wa kujitoa. Karibu tushiriki Baraka hii kwa pamoja.
Katika huduma hii ya vijijini sina namna, nawe ni shahidi maisha ya watu wanoishi huko vijijini yalivyo, ni duni mno, jamani ukiyaona hutatamani kwenda ukae huko. Lakini niwatu wa Mungu wale  wanahitaji injili kama inavyotakiwa pande zote duniani.
Ninatamani nikiwa naenda kwenye Injili vijijini huku nawapelekea misaada walau kidogo kwa kile ambacho watu wa Mungu mtakuwa mnanipa kukipeleka kwa watu hao.
Nia yangu, na moyo wangu ni Injili  iwashe moto mioyo ya watu wa vijijini. Mambo yanayofanyika vijijini ni aibu, watoto wanabakwa jamani, miaka mitatu, na kupanda, ndoa zinavunjika vibaya mno, hakuna amani zaidi ya majuto unajua ni kwanini?
Soma Rumi 1:28,  “Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.”  Unaona lakini ukifuatilia juujuu utasema ndivyo ilivyo, nami nakuuliza swali fahamu zao zimefundishwa au kuuelekezwa na nani aliyejitoa kwenda kwao?
Mtu hawezi kukataa asichoambiwa, bali hukataa anachoambiwa je ndugu zetu hawa wameambiwa na nani mpaka wakatae au wakubali?
Soma kwa makini sura hii Rumi 10:13-15  “kwa kuwa, kila atakaye liitia jina la Bwana ataokoka”
Biblia iko wazi kabisa kila atakaye kuwa wazi kumuita bwana  ataokolewa. Swali ni hili naomba mimi na wewe tulijibu “basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije wasipoperekwa?...”  
shida sio kuhubiri, shida sio ujumbe shida ni muhubiri.
Nami leo nakataa kuwa shida sio Mhubili kwa sababu mimi nipo tayali kwenda shida ni hii NANI WA KUNIPELEKA HUKO?
Mpendwa nipereke ili tuishiriki baraka hii ya kristo. Unacho cha kupereka nami nimeereza kwenye mchanganuo wa mahitaji ya Injili kama ifuatavyo.

WATU
  • Waombaji
  • Watafiti wa maeneo ambayo hayajafikiwa ili tuyape kipaumbele kuyafikia.
  • Waimbaji
  • Wafuatiliaji baada ya watu kuokoka.
MALI NA FEDHA.
  •  Pesa tasilimu
  • Mali na vitu mbalimbali kama vile Nguo, viatu, chakula na chochote ambacho Mungu atkujalia.
VIFAA VYA INJILI
  • Vyombo vya injili kama generator, spika nk
  • Usafili kama gari, kutusafirisha, nk
  • Jukwaa la kutembea nalo
  • mahema ya pale tutakapo weka kambi. nk
Bwana Yesu  apewe sifa sana. mpendwa vitu ni vingi mno lakini kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Kama uko tayali. Kwa mawasiliano, ushauri, kujitoa naomba uwasiliane na mimi kwa
Namba zifuatazo
Ev Peter Kamanija
0757-537232
0787-537232








KUWA MAKINI NA MAFUNDISHO YA UONGO


KUWA MAKINI NA MAFUNDISHO YA UONGO.
Na Peter Kamanija.
Wapendwa Nawasalimu Katika Jina La Yesu.
Namshukuru sana Mungu kunipa nafasi hii ya kuongea na wewe kwa njia hii ya maandishi. Pia asante sana kwa kutoa Muda wako Kusoma ujumbe huu, ni maombi yangu makubwa sana kwa Mungu kwamba unaposoma Ujumbe huu Mungu akufundishe zaidi na zaidi, ili uweze kukua katika wokovu na kumjua Yesu Kristo, na zaidi sana tufike Mbinguni kwa Ushindi Mkubwa. Karibu uwe nami sasa katika somo hili.
Lengo la kuandika ujumbe huu ni kwa ajili ya kuitetea na kuilinda imani tuliyokabidhiwa mara moja tu, dhidi ya mafundisho ambayo yanakuja kasi na kuwakumba hata yamkini wateule. Yuda 1:3-4, 1Timotheo 1:18, 1Petro 1:5. Baada ya kukabidhiwa imani na maneno haya hatuna budi kuyalinda kwa gharama yoyote ile dhidi ya mafundisho potofu iwe ni kwa kujua ama kwakutokujua kwa anaye fundisha. Lazima Neno la Mungu lifundishwe kwa usahihi wake.
Kuna mafundisho ambayo yamekuwa yakifundishwa kinyume na Biblia. Mafundisho hayo ni mengi mno mfano; wanasema  “kuokoka tu hakutoshi inatakiwa ukombolewe”, “kuvunjiwa laana” na  “maombi ya utakaso wa jina la yesu” luka 11:2. “akawaambia, Msalipo semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], jina lako litakaswe, ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni.] katika ujumbe huu tuangalie mada moja inayosema “maombi ya utakaso wa jina la yesu” leon naomba nianze na fundisho hili.
A.    MAOMBI YA UTAKASO WA JINA LA YESU.
wanasema “ katika maombi nilazima ulitakase kwanza Jina la Yesu, mapepo hayatoki kwa sababu Jina la Yesu limechafuliwa na linakuwa chafu,  na mahitaji yetu hatupokei kwasababu Jina hili lina kuwa limechafuka, sasa ili kupata majibu na kufunguliwa ni lazima tulitakase kwanza Jina la Yesu, liwe safi ndipo, tulitumie”
Waalimu wa masomo hayo japokuwa wanaeleza na kufundisha mambo mingine vizuri. Lakini tunaona kuwa kichwa cha habari ni cha muhimu sana na ndicho sikuzote kinachoelezea ujumbe mzima wa mwalimu. Mwalimu yoyote ni lazima aweke wazi kichwa cha habari ili kuwaweka wanafunzi kuwa makini na ujumbe wake.Vivyo hivyo hata kwa waalimu hawa wanaweka vichwa vya habari vizuri kwa macho lakini vyenye utata mkubwa sana na kutokueleweka vizuri kwa watu, na mafundisho yao huwa na utata kwa wasikilizaji na washirika kwa ujumla.
Na mafundisho hayo ndiyo yalilowasha Moyo wangu katika kutetea na kusema ukweli wa Injili kuhusu, Jina la Yesu sawasawa na Biblia isemavyo.  ‘HAIKUTOKEA, HAIJATOKEA NA WALA HAITAKUJA KUTOKEA JINA LA YESU KRISTO ALIYE HAI KUTAKASWA’ kwanini nakataa kwa sababu Biblia imekaa kimya katika fundisho hilo kama ifuatazo.
1.      Mungu ni mtakatifu sana.
Mungu ni mtakatifu na katika utakatifu huo alimwagiza mwanadamu awe mtakatifu kama yeye alivyo mtakatifu. 1Petro 1:15-16. Kama YEYE ALIYEWAITA ALIVYO MTAKATIFU ninyi nanyi iweni watakatifu. Iweje tulitakase jina la yeye aliye mtakatifu? Iweje tulitakase jina la yeye aliyetuita? Je si kukufuru huku? Hili ni tusi, ni kumtukana Mungu. Mungu atusaidie sana wapendwa na atusamehe. Tuwe makini mno kwa kila fundisho. Soma tena mwenyewe. Walawi 11:44-45, 19:2, Isaya 43:3, 1Thesalonike 4:7.
2.      Jina lake Ni Takatifu Sana, hivyo hutakasa mwenyewe jina lake kwa ajili yetu. Hutusaidia mwenyewe. Na kama kwa namna moja au nyingine limechafuliwa na hasa huchafuliwa kwa dhambi zetu na maovu yetu. Yeye huingilia kati na kutakasa na kuludisha heshima ya Jina Lake Takatifu. Ezekieli 36:22-23, “ …nami nitalitakasa JINA LANGU KUU,…” Eze 20:44. Je kulitakasa Jina lake si kuingilia kazi yake? Sisi tunaweza kuwa sawa na Mungu kweli mpaka tufikie mahali pa kulitakasa jina lake?
3.      Yesu alipewa Jina lipitalo Majina yote. Wafilipi 2:9, Efeso 1:21,
Jina la Yesu ni jina lenye nguvu, ni jina lililo juu ya majina yote, Juu ya vitu vyote. Kama Ndivyo Mimi ni Nani hata nidiriki kulitakasa Jina ambalo kwa hilo lazima nilipigie Magoti? Hapana siko tayali kulidharau Jina la Bwana wangu kiasi hicho. Asomaye na afahamu.
4.      Jina la Yesu limebeba ukombozi kamili.
a.       Mathayo 1:21, “ naye atazaa mwana, nawe utamwita Jina lake Yesu, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao” sisi ni watu wa Yesu, tuliompokea Yesu ni watoto wake. Yohana 1:12. Sasa kama ndivyo iweje tulio watoto wa Yesu Kristo tutakase Jina lake yeye aliyetufanya sisi kuwa wana? Luka 1:31, 2:21. Iweje tulitakase Jina la yesu, ambalo Mungu kampa mwanawe?
b.      Ni Jina liokoalo Matendo 4:12, tulipewa jina la Yesu kwani ndilo linalopaswa kutuokoa sisi. Matendo 2:21 kila atakaye liitia jina la Bwana ataokolewa. Rumi 10:13, Yoeli 2:32, Zaburi 50:15. Iweje jina liokoalo liwe chafu? Iweje niokolewe na Jina lisilo kuwa na uwezo wa kujitakasa lenyewe? Kuna umaana gani wa kuliitia jina ambalo ninauwezo wa kulitakasa? Ndugu yangu Jina la Yesu linajitegemea, lina uwezo mzito na Nguvu kubwa, uwezo wake uko juu sana kuliko mamlaka zote na usultani hatupaswi kabisa hata kutamka kwamba eti tulitakase.
5.      Sisi ndio tuliotakaswa katika Kristo.1Korintho 6:11, 1Korintho 1:2, Biblia ikowazi kabisa kwamba sisi tulitakaswa katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Je Jina linaloweza kututakasa leo linaweza kubeba uchafu tena alafu tukalitakasa sisi tuliotakaswa kupitia Jina Hilo?
6.      Tumepewa kulihubiri Jina Lake katikati ya Mataifa. Ebrania 2:11-12, Zaburi 22:22, Yohana 20:17. Mungu ni Mtakatifu sana na kila amwendeaye Mungu lazima ajitakase ndipo amkaribie Mungu na kuongea naye. Sasa je iweje tulihubiri jina ambalo linaweza kuchafuka? Je watu wanaweza kuliamini jina hilo tunapolihubili au ndio tutaongeza maswali Mengi kwa watu na kutokuliamini? Hapana Jina La Yesu ni takatifu sana wala halitakuja kuchafuka maishani. Jina LaYesu Ni Safi mno kama yeye Alivyo Msafi kupita kawaida.
7.      Tumeambiwa tuombe lolote kwa Jina LakeYesu. Yohana 14:14, Yohana 16:23-24, 1Yohana 5:14. Maagizo ya Bwana Wetu Yesu Kristo ni kuomba lolote kwa Jina lake. Tafadhali  naomba Niulize je Yesu angeweza kutuambia Tuombe kwa Jina lake na Huku anajua kabisa Mungu hamsikilizi Mtu mwovu, Iweje tutumie Jina ambalo linaweza kuchukua Uovu kumkaribia Mungu aliye Mtakatifu?
Ndugu yangu mpendwa naomba ufahamu kuwa fundisho hilo ni kumkufuru Mungu, Roho Mtakatifu na Yesu Mwenyewe, kwa lugha nyepesi ni tusi kwa Mungu Msafi. Mimi mwanadamu nisiyefaa kabisa leo niende kulitakasa Jina la yeye aliye Mtakatifu kuliko mimi? Kwa haki gani niliyonayo? Kwa umaarufu gani nilionao? Sisi tumeokolewa kwa neema hatukustahili kabisa, Lakini Yesu kwa kutupenda akaja kwetu, akatuokoa na kila kitu kwake ni kikamailifu. Wapendwa kila aliye na matumaini kwa Kristo hujitakasa 1Yohana 3:3. Turudi tumeenda mbali sana. Tutubu kabisa, na kuomba Rehema kwa Mungu hata kwa kusikia kwetu tu hili jambo, hata kwa kulisoma tuombe Rehema za Mungu juu yetu.
TULIANGALIE HILI ANDIKO KWA UNDANI.
Katika Biblia ya Kiswahili imetafsiriwa kutoka ile lugha ya kiingereza cha kale, na ile ya kiingereza imetafsiriwa toka lugha ya kiebrania na kiyunani cha kale. Na siku zote tunaona lugha ikitafsiliwa jumbe huwa ni zilezile kuwakilishwa kukawa tofauti. Japokuwa maana inakuwa ni ileile. Dawa ya hapo sio kusema Biblia imekosewa bali ni kurudi katika kanuni ya kutafsiri maandiko, na hapo ndipo tutakapoupata ule ukweli wake wote, na uharisia wake.
Sintaweza kueleza kanuni ya kutafsiri Biblia kwani sio mahari pake hasa. Ila turudi katika chimbuko la neno ambalo lilisimamiwa na hili  fundisho tuone maana halisi ya Yesu aliposema hivyo alimaanisha nini.

Fuatilia kwa makini jedwali hili hapa chini na maelezo yake tuone.
S/N
Aina ya Biblia
Maana Kwa Kiingereza
Maana kwa Kiswahili.


Luka 11:2.
Mathayo 6:9
Maana ni Moja.
1.
King James Version
“And he said unto them, When ye pray, say, Our Father which art in heaven, Hallowed be thy name, Thy kingdom come. Thy will be done, as in heaven, so in earth.
After this manner therefore pray ye: Our Father which art in heaven, Hallowed be thy name.
“Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako Litukuzwe”
2.
New International version
He said to them “when you pray, say: ‘Father, hallowed be your name, your kingdom come…’”
This is how you should pray: “ ‘Our Father in heaven, hallowed be your name, …’ ”
Mnapo omba semeni: “Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe…”
3.
*HCSB.
He said to them “Whenever you pray, say: Father your name be honored as holy. Your kingdom come.
“Therefore, you should pray like this: Our Father in heaven your name be honored as holy.
“kwa hiyo Ombeni hivi ‘Baba yetu uliye mbinguni Jina lako liheshimiwe kama takatifu’
*HCSB – Holman Christian Standard Bible.
Umeona; ukiangalia katika tafsiri zote tatu za kiingereza utaona kuwa maneno ni yaleyale na maana ni ileile ya kuomba “Baba yetu Uliye Mbinguni Jina Lako Litukuzwe”
Ndugu yangu mpendwa tafadhali usije ukajaribu hata kuthubutu kulitakasa Jina la Yesu. Hakuna sehemu yoyote katika Biblia walipoagizwa hata mitume au manabii hata Musa mwenyewe hakuwahi kuambiwa atakase Jina La Bwana hakuna.
Angalizo: Watumishi wa Mungu Tafadhali Tuwe makini sana katika kuandaa Jumbe Zetu. Andiko lolote ambalo halina andiko lingine kama hivi hili la Luka Lisitawale kuwa ndilo fundisho. Hebu fundisho letu libebwe na maandiko mengi yanayobeba ujumbe tunaohitaji kuufundisha.
Na pia washirika wa makanisani Baraka zako na Muujiza wako uko hapohapo kanisani, na kwa huyohuyo Mchungaji wako. Acha kabisa kukimbilia kimbilia kuwekewa mikono. Utapewa na ma-roho mengine alafu yatakutesa katika maisha yako.
Ndugu zangu wapenzi nawashukuru sana kwa kuwa nami na Mungu awabariki kwa Baraka zote za kimwili na Kiroho pia naomba tufuatane pamoja katika somo la pili ni muhimu mno kulifahamu. Linaitwa KUVUNJA LAANA.
Nawatakia mafanikio mema katika kazi na katika utumishi.
KWA MAWASILIANO ZAIDI.
Kwa ajili ya semina, mkutano wa injili, na mafundisho mengine wasiliana nasi.
Believe The Gospel.
Peter & Natalia Kamanija.
SIMU: 0757-537232, 0757-526846, 0787-537232.

FUATILIA KWA UMAKINI BLOG HII UWEZE KUPOKEA UPONYAJI



Powered by Blogger.

www.CodeNirvana.in

Pages

© Copyright BELIEVE THE GOSPEL
Back To Top