KUWA
MAKINI NA MAFUNDISHO YA UONGO.
Na Peter Kamanija.
Wapendwa Nawasalimu Katika Jina La Yesu.
Namshukuru sana Mungu kunipa nafasi hii
ya kuongea na wewe kwa njia hii ya maandishi. Pia asante sana kwa kutoa Muda
wako Kusoma ujumbe huu, ni maombi yangu makubwa sana kwa Mungu kwamba unaposoma
Ujumbe huu Mungu akufundishe zaidi na zaidi, ili uweze kukua katika wokovu na
kumjua Yesu Kristo, na zaidi sana tufike Mbinguni kwa Ushindi Mkubwa. Karibu
uwe nami sasa katika somo hili.
Lengo la kuandika ujumbe huu ni kwa
ajili ya kuitetea na kuilinda imani tuliyokabidhiwa mara moja tu, dhidi ya
mafundisho ambayo yanakuja kasi na kuwakumba hata yamkini wateule. Yuda 1:3-4,
1Timotheo 1:18, 1Petro 1:5. Baada ya kukabidhiwa imani na maneno haya hatuna
budi kuyalinda kwa gharama yoyote ile dhidi ya mafundisho potofu iwe ni kwa
kujua ama kwakutokujua kwa anaye fundisha. Lazima Neno la Mungu lifundishwe kwa
usahihi wake.
Kuna mafundisho ambayo yamekuwa yakifundishwa
kinyume na Biblia. Mafundisho hayo ni mengi mno mfano; wanasema “kuokoka tu hakutoshi inatakiwa ukombolewe”,
“kuvunjiwa laana” na “maombi ya utakaso
wa jina la yesu” luka 11:2. “akawaambia, Msalipo semeni, Baba [yetu uliye
mbinguni], jina lako litakaswe, ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe hapa
duniani kama huko mbinguni.] katika ujumbe huu tuangalie mada moja inayosema “maombi
ya utakaso wa jina la yesu” leon naomba nianze na fundisho hili.
A. MAOMBI YA UTAKASO WA JINA LA YESU.
wanasema “ katika maombi nilazima
ulitakase kwanza Jina la Yesu, mapepo hayatoki kwa sababu Jina la Yesu
limechafuliwa na linakuwa chafu, na
mahitaji yetu hatupokei kwasababu Jina hili lina kuwa limechafuka, sasa ili
kupata majibu na kufunguliwa ni lazima tulitakase kwanza Jina la Yesu, liwe
safi ndipo, tulitumie”
Waalimu wa masomo hayo japokuwa wanaeleza
na kufundisha mambo mingine vizuri. Lakini tunaona kuwa kichwa cha habari ni
cha muhimu sana na ndicho sikuzote kinachoelezea ujumbe mzima wa mwalimu.
Mwalimu yoyote ni lazima aweke wazi kichwa cha habari ili kuwaweka wanafunzi
kuwa makini na ujumbe wake.Vivyo hivyo hata kwa waalimu hawa wanaweka vichwa
vya habari vizuri kwa macho lakini vyenye utata mkubwa sana na kutokueleweka
vizuri kwa watu, na mafundisho yao huwa na utata kwa wasikilizaji na washirika
kwa ujumla.
Na mafundisho hayo ndiyo yalilowasha
Moyo wangu katika kutetea na kusema ukweli wa Injili kuhusu, Jina la Yesu sawasawa
na Biblia isemavyo. ‘HAIKUTOKEA,
HAIJATOKEA NA WALA HAITAKUJA KUTOKEA JINA LA YESU KRISTO ALIYE HAI KUTAKASWA’ kwanini
nakataa kwa sababu Biblia imekaa kimya katika fundisho hilo kama ifuatazo.
1. Mungu ni mtakatifu sana.
Mungu ni
mtakatifu na katika utakatifu huo alimwagiza mwanadamu awe mtakatifu kama yeye
alivyo mtakatifu. 1Petro 1:15-16. Kama YEYE ALIYEWAITA ALIVYO MTAKATIFU ninyi
nanyi iweni watakatifu. Iweje tulitakase jina la yeye aliye mtakatifu? Iweje
tulitakase jina la yeye aliyetuita? Je si kukufuru huku? Hili ni tusi, ni
kumtukana Mungu. Mungu atusaidie sana wapendwa na atusamehe. Tuwe makini mno
kwa kila fundisho. Soma tena mwenyewe. Walawi 11:44-45, 19:2, Isaya 43:3,
1Thesalonike 4:7.
2.
Jina lake Ni
Takatifu Sana,
hivyo hutakasa mwenyewe jina lake kwa ajili yetu. Hutusaidia mwenyewe. Na kama
kwa namna moja au nyingine limechafuliwa na hasa huchafuliwa kwa dhambi zetu na
maovu yetu. Yeye huingilia kati na kutakasa na kuludisha heshima ya Jina Lake
Takatifu. Ezekieli 36:22-23, “ …nami nitalitakasa JINA LANGU KUU,…” Eze 20:44.
Je kulitakasa Jina lake si kuingilia kazi yake? Sisi tunaweza kuwa sawa na
Mungu kweli mpaka tufikie mahali pa kulitakasa jina lake?
3.
Yesu alipewa
Jina lipitalo Majina yote. Wafilipi 2:9, Efeso 1:21,
Jina la Yesu ni
jina lenye nguvu, ni jina lililo juu ya majina yote, Juu ya vitu vyote. Kama
Ndivyo Mimi ni Nani hata nidiriki kulitakasa Jina ambalo kwa hilo lazima nilipigie
Magoti? Hapana siko tayali kulidharau Jina la Bwana wangu kiasi hicho. Asomaye
na afahamu.
4. Jina la Yesu limebeba ukombozi kamili.
a.
Mathayo
1:21, “ naye atazaa mwana, nawe utamwita Jina
lake Yesu, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao”
sisi ni watu wa Yesu, tuliompokea Yesu ni watoto wake. Yohana 1:12. Sasa kama
ndivyo iweje tulio watoto wa Yesu Kristo tutakase Jina lake yeye aliyetufanya
sisi kuwa wana? Luka 1:31, 2:21. Iweje tulitakase Jina la yesu, ambalo Mungu
kampa mwanawe?
b.
Ni Jina liokoalo Matendo 4:12,
tulipewa jina la Yesu kwani ndilo linalopaswa kutuokoa sisi. Matendo 2:21 kila
atakaye liitia jina la Bwana ataokolewa. Rumi 10:13, Yoeli 2:32, Zaburi 50:15.
Iweje jina liokoalo liwe chafu? Iweje niokolewe na Jina lisilo kuwa na uwezo wa
kujitakasa lenyewe? Kuna umaana gani wa kuliitia jina ambalo ninauwezo wa
kulitakasa? Ndugu yangu Jina la Yesu linajitegemea, lina uwezo mzito na Nguvu
kubwa, uwezo wake uko juu sana kuliko mamlaka zote na usultani hatupaswi kabisa
hata kutamka kwamba eti tulitakase.
5.
Sisi ndio
tuliotakaswa katika Kristo.1Korintho 6:11, 1Korintho 1:2, Biblia
ikowazi kabisa kwamba sisi tulitakaswa katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
Je Jina linaloweza kututakasa leo linaweza kubeba uchafu tena alafu
tukalitakasa sisi tuliotakaswa kupitia Jina Hilo?
6.
Tumepewa
kulihubiri Jina Lake katikati ya Mataifa. Ebrania 2:11-12, Zaburi 22:22,
Yohana 20:17. Mungu ni Mtakatifu sana na kila amwendeaye Mungu lazima ajitakase
ndipo amkaribie Mungu na kuongea naye. Sasa je iweje tulihubiri jina ambalo
linaweza kuchafuka? Je watu wanaweza kuliamini jina hilo tunapolihubili au ndio
tutaongeza maswali Mengi kwa watu na kutokuliamini? Hapana Jina La Yesu ni
takatifu sana wala halitakuja kuchafuka maishani. Jina LaYesu Ni Safi mno kama
yeye Alivyo Msafi kupita kawaida.
7.
Tumeambiwa
tuombe lolote kwa Jina LakeYesu. Yohana 14:14, Yohana 16:23-24, 1Yohana
5:14. Maagizo ya Bwana Wetu Yesu Kristo ni kuomba lolote kwa Jina lake. Tafadhali naomba Niulize je Yesu angeweza kutuambia
Tuombe kwa Jina lake na Huku anajua kabisa Mungu hamsikilizi Mtu mwovu, Iweje
tutumie Jina ambalo linaweza kuchukua Uovu kumkaribia Mungu aliye Mtakatifu?
Ndugu yangu mpendwa naomba ufahamu kuwa
fundisho hilo ni kumkufuru Mungu, Roho Mtakatifu na Yesu Mwenyewe, kwa lugha
nyepesi ni tusi kwa Mungu Msafi. Mimi mwanadamu nisiyefaa kabisa leo niende
kulitakasa Jina la yeye aliye Mtakatifu kuliko mimi? Kwa haki gani niliyonayo?
Kwa umaarufu gani nilionao? Sisi tumeokolewa kwa neema hatukustahili kabisa,
Lakini Yesu kwa kutupenda akaja kwetu, akatuokoa na kila kitu kwake ni
kikamailifu. Wapendwa kila aliye na matumaini kwa Kristo hujitakasa 1Yohana 3:3.
Turudi tumeenda mbali sana. Tutubu kabisa, na kuomba Rehema kwa Mungu hata kwa
kusikia kwetu tu hili jambo, hata kwa kulisoma tuombe Rehema za Mungu juu yetu.
TULIANGALIE HILI ANDIKO KWA UNDANI.
Katika Biblia ya Kiswahili imetafsiriwa
kutoka ile lugha ya kiingereza cha kale, na ile ya kiingereza imetafsiriwa toka
lugha ya kiebrania na kiyunani cha kale. Na siku zote tunaona lugha ikitafsiliwa
jumbe huwa ni zilezile kuwakilishwa kukawa tofauti. Japokuwa maana inakuwa ni
ileile. Dawa ya hapo sio kusema Biblia imekosewa bali ni kurudi katika kanuni
ya kutafsiri maandiko, na hapo ndipo tutakapoupata ule ukweli wake wote, na
uharisia wake.
Sintaweza kueleza kanuni ya kutafsiri
Biblia kwani sio mahari pake hasa. Ila turudi katika chimbuko la neno ambalo
lilisimamiwa na hili fundisho tuone maana
halisi ya Yesu aliposema hivyo alimaanisha nini.
Fuatilia kwa makini jedwali hili hapa
chini na maelezo yake tuone.
S/N
|
Aina ya Biblia
|
Maana Kwa
Kiingereza
|
Maana kwa Kiswahili.
|
|
|
Luka
11:2.
|
Mathayo
6:9
|
Maana
ni Moja.
|
1.
|
King
James Version
|
“And
he said unto them, When ye pray, say, Our Father which art in heaven,
Hallowed be thy name, Thy kingdom come. Thy will be done, as in
heaven, so in earth.
|
After
this manner therefore pray ye: Our Father which art in heaven,
Hallowed be thy name.
|
“Baba
yetu uliye mbinguni, Jina lako Litukuzwe”
|
2.
|
New
International version
|
He
said to them “when you pray, say: ‘Father, hallowed be your name,
your kingdom come…’”
|
This
is how you should pray: “ ‘Our Father in heaven, hallowed be
your name, …’ ”
|
Mnapo
omba semeni: “Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe…”
|
3.
|
*HCSB.
|
He
said to them “Whenever you pray, say: Father your name be honored as holy.
Your kingdom come.
|
“Therefore,
you should pray like this: Our Father in heaven your name be
honored as holy.
|
“kwa
hiyo Ombeni hivi ‘Baba yetu uliye mbinguni Jina lako liheshimiwe kama
takatifu’
|
*HCSB – Holman Christian Standard Bible.
Umeona; ukiangalia katika tafsiri zote
tatu za kiingereza utaona kuwa maneno ni yaleyale na maana ni ileile ya kuomba “Baba
yetu Uliye Mbinguni Jina Lako Litukuzwe”
Ndugu yangu mpendwa tafadhali usije
ukajaribu hata kuthubutu kulitakasa Jina la Yesu. Hakuna sehemu yoyote katika
Biblia walipoagizwa hata mitume au manabii hata Musa mwenyewe hakuwahi kuambiwa
atakase Jina La Bwana hakuna.
Angalizo: Watumishi wa Mungu Tafadhali
Tuwe makini sana katika kuandaa Jumbe Zetu. Andiko lolote ambalo halina andiko
lingine kama hivi hili la Luka Lisitawale kuwa ndilo fundisho. Hebu fundisho
letu libebwe na maandiko mengi yanayobeba ujumbe tunaohitaji kuufundisha.
Na pia washirika wa makanisani Baraka
zako na Muujiza wako uko hapohapo kanisani, na kwa huyohuyo Mchungaji wako.
Acha kabisa kukimbilia kimbilia kuwekewa mikono. Utapewa na ma-roho mengine
alafu yatakutesa katika maisha yako.
Ndugu zangu wapenzi nawashukuru sana kwa
kuwa nami na Mungu awabariki kwa Baraka zote za kimwili na Kiroho pia naomba
tufuatane pamoja katika somo la pili ni muhimu mno kulifahamu. Linaitwa KUVUNJA
LAANA.
Nawatakia mafanikio mema katika kazi na
katika utumishi.
KWA
MAWASILIANO ZAIDI.
Kwa ajili ya semina, mkutano wa injili, na
mafundisho mengine wasiliana nasi.
Believe
The Gospel.
Peter
& Natalia Kamanija.
SIMU:
0757-537232, 0757-526846, 0787-537232.